Select Page

Tatizo La UWASILISHAJI Linasumbua Hadi Wasomi

Written by Shukuru Amos

Tanzania's most followed marketer on LinkedIn. Content Alchemist; building and executing content strategies for B2B brands, Founders and Solopreneurs.

Kwenye post hii pale LinkedIn, kuna watu kadhaa wamejaribu kukosoa lugha niliyotumia. Huwa napata critics hizi mara nyingi. Watu hawa hawajui mimi ni mwalimu wa lugha na fasihi na kwa miaka mingi nimethibitisha umahiri katika eneo hili la uwasilishaji. What they miss is why nimechagua aina hii ya uwasilishaji.

 

Moja kati ya sanaa zinaogopwa na mamlaka dhalimu ni mziki wa kufoka. Nay wa Mitego akiimba kuhusu uongozi mbovu lazima nyimbo ifungiwe. Roma yuko mafichoni.

Kwanini? Ukitaka kupata mrejesho kwa watu, ukitaka watu waamke na wachukue hatua, lazima ujumbe wako uibue hisia za kero na mshituko. The average mwananchi is docile. Ukiwasilisha kipole, kizembe, na kitakatifu utaishia kupata “Well said” na “Spot on”.

Yesu mwenyewe inafika mahali anaita watu wapumbavu, wanafiki, na waongo. Anaenda mbali anakuwa violent anavuruga meza za biashara ndani nyumba yake. Kama Yesu hakubembelezi, itakuwa mimi?

Most people have barely scratched the surface of effective delivery. 

Wengine wasomi kabisa. Sijui wanapataje hizo Dr. na PhD bila kusoma rhetoric. Au ni za “kutunukiwa”. Tatizo la wengi, hasa wazee ni wamekua enzi za Nyerere zilizotawaliwa na uoga pamoja na maonyo makali.

Waliosoma kitabu changu wanaelewa. Nimetumia kurasa nyingi kueleza saikolojia ya maudhui na kitu kinaitwa “signaling”. Mfano wa signaling; mimi siwezi kusema kuwa nina ujasiri. Ila nitaongelea kitu ambacho wewe umefyata mkia kukiongelea. Hapo ndipo utakiri kimoyo moyo “this guys is confident.”

The best way to convey reality in a way that will shock people is to weave it into art and fiction. 

Yesu Kristo na kushtua watu

Halikuwa jambo geni kwa miungu wa zamani kupata shida na matatizo ya kibinadamu. Mengine kupelekea kufa kwao. Lakini walipata matatizo hayo wakiwa kwenye hali ya umungu. They remained in their god ranks. Hivyo, ikawa vigumu kwa watu ku-relate ni kwa kiasi gani miungu hao waliteseka. Kama mtu si sehemu ya uhalisia wako, unakosa muktadha unaokuruhusu uhisi shida zake.

Lakini aliyekuja kuwastua wanadamu na kuwakera baadhi ni Yesu. Yaani akajishusha hadi kuwa binadamu wa kawaida. Tena maskini. Huo mshitko wa kwanza. Na kero kwa Warumi maana walitarajia mfalme dikteta. 

Isitoshe akauawawa na wanajeshi watumwa wa Roma. Mshituko wa pili kwa watu. Kilichofuata ni wafuasi wake kumwanini zaidi na kufanya msalaba kuwa alama ya utukufu na utakatifu. Huu nao ni mshangao na mshituko kwani msalaba ilikuwa alama ya mateso kwa watu wa chini kabisa katika jamii. Watu wa kutupwa.

Hapa ninajaribu kukuonyesha umuhimu wa kuchombeza mshangao, kero, mshituko na sanaa kwenye ujumbe wako. Yesu aliingia kwa kushangaza watu (Mungu gani anazaliwa zizini?) na kuondoka kwa kustua wengi. Mpaka leo, neno la Yesu linatamkwa katika kila kinywa. Waamini na wasioamini.

Uwasilishaji fanisi umekaa kichokozi

Wale wanaonikosoa ndiyo uthibitisho wa hoja yangu. Kwa maana huwa siwaoni wakishiriki kwenye post zingine. Lakini ujumbe wangu umewastua kiasi cha kuacha comment. Ningetumia lugha ya kawaida wangepita tu. Post zangu nyingi zinazoanzisha mijadala ya maana ni zile ambazo nimetia uchizi na uchokozi kwenye uwasilishaji.

Subscribe to my Agency Newsletter

Join over 500 others getting the best of our advice.